Kariakoo_TacticsYoung Africans
20 Sept 2026Uchambuzi wa Mbinu
Bora kati ya Fiston Mayele na Meddie Kagere: Nani straika hatari zaidi aliyewahi kutua VPL?
Kagere alifunga mabao muhimu sana kwa misimu miwili mfululizo na kubeba viatu vya ufungaji bora. Mayele akaja na style yake ya kutetema na kufunga mabao ya maamuzi. Nani alikuwa tishio zaidi kwa mabeki wa ligi?
Mawazo ya Wana-Kijiwe2
Kagere alikuwa mnyama ndani ya 18! Hata akipata nusu nafasi ilikuwa goli. Mayele alikuwa mzuri pia lakini Kagere alikuwa mtulivu zaidi kwenye mechi kubwa.
Mayele hakuwa anafunga tu, alikuwa anatesa safu nzima ya ulinzi na kutoa pasi za mwisho. Yule jamaa alikuwa complete striker.