Balozi_Wa_SokaTanzania
20 Sept 2026Uchambuzi wa Mbinu
Je, vilabu vyetu vina uwezo wa kucheza Fainali ya CAF Champions League msimu huu?
Kila mwaka tunafika robo fainali na kuishia hapo kwa tofauti ndogo za uzoefu dhidi ya Waarabu (Al Ahly, Mamelodi Sundowns, ES Tunis). Ni kipi kinachokosekana sasa hivi ili kuingia hatua ya fainali na kubeba taji?
Mawazo ya Wana-Kijiwe4
Kinachokosekana ni uimara wa safu ya ulinzi mechi za ugenini. Nyumbani tunacheza vizuri sana mbele ya mashabiki 60,000, lakini ugenini tunarudi nyuma sana.
Kama mshabiki wa Kenya, lazima niseme soka la Tanzania linazidi kupaa. Ushindani wa Simba na Yanga kimataifa unaleta heshima kubwa kwa ukanda wetu wa CECAFA.
Hii mada ni moto sana! Hata hivyo takwimu zinaonyesha Yanga wako vizuri.
Nakubaliiii